Ubingwa wa kombe la FA waharibu mipango yote klabuni Chelsea - Darajani 1905

Ubingwa wa kombe la FA waharibu mipango yote klabuni Chelsea

Share This

Mpaka sasa Chelsea ndio moja ya klabu chache barani Ulaya ambayo haijatoa ratiba kamili ya michezo ya kirafiki ya kujiandaa na msimu mpya ujao licha ya hapo kabla kutoa ratiba ambayo inaonekana itavurugika haswa kutokana na ubingwa ilioshinda ikiibamiza Manchester united kwenye mchezo wa fainali ya kombe la FA mwezi May.

Ni mchezo mmoja tu ambao unaonekana kuwa wa uhakika ambao ni dhidi ya Perthy Glory utakaochezwa tarehe 23-Julai huko nchini Australia kwenye uwanja mpya ambapo Chelsea itakuwa ni kama inaufungua rasmi.

Lakini michezo mingine iliyopangwa hapo kabla ni kama itabadilika ratiba na viwanja vya kuchezea.

Moja ya michezo hiyo ni mchezo wa kirafiki dhidi ya Arsenal ambao mwanzoni ulipangwa kuchezwa tarehe 4-Agosti huko nchini Sweden lakini kutokana na ubingwa wa Chelsea wa kombe la FA basi itamaanisha klabu hiyo itacheza mchezo wa Ngao ya Hisani dhidi ya bingwa wa ligi kuu, Manchester city uliopangwa kuchezwa tarehe 5-Agosti.

Kutokana na ratiba ilivyo ni kama leo ikicheza na Arsenal basi kesho itacheza na Man city kwenye mchezo huo wa Ngao ya Hisani jambo ambalo haliwezekani na hivyo kuamriwa mchezo wa dhidi ya Arsenal kupelekwa mpaka tarehe 1-Agosti na utachezwa huko Dublin kwenye uwanja wa Aviva nchini Ireland.

Mchezo mwengine ni dhidi ya Sevilla ambao ulipangwa kuchezwa tarehe 28-Julai lakini kutokana na ratiba ya ligi ya Ulaya (Europa League) kuingiliana na mchezo huo basi mchezo huo unaweza kubadilishwa tarehe. Mchezo wa tatu ni dhidi ya Inter Milan ambao mwanzoni ulipangwa kuchezwa tarehe 1-Agosti lakini nao unadhaniwa kwamba unaweza kubadilishwa tarehe.

No comments:

Post a Comment