Klabu za Real Madrid na Barcelona zimekuwa zikitajwa mara kadhaa kumfukuzia nyota wa klabu ya Chelsea raia wa Ubelgiji, Eden Hazard.
Lakini kuna taarifa ambazo zinaweza kuwa nzuri kwa mashabiki wa Chelsea, kuna ripoti zinasema uongozi wa klabu ya Chelsea umejiandaa kupinga ofa yoyote inayoletwa ili kusajiliwa kwa nyota huyo aliyeiongoza vyema timu yake ya taifa ya Ubelgiji kwenye michuano ya Kombe la Dunia ambako huko wamemaliza kwenye nafasi ya mshindi wa tatu.
Real Madrid ndio klabu inayotajwa kwa karibu kumfukuzia nyota huyo aliyedumu klabuni Chelsea kwa miaka sita sasa ambapo alisajiliwa akitokea klabu ya Lille ya nchini Ufaransa.
Kuondoka kwa Cristiano Ronaldo klabuni Real Madrid kunatajwa kuichochea klabu hiyo kumfukuzia nyota huyu.
Pia unaweza kupata muhtasari wa habari za Chelsea, kupitia kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment