Golovin azidisha vita ya Emenalo dhidi ya Chelsea - Darajani 1905

Golovin azidisha vita ya Emenalo dhidi ya Chelsea

Share This

Nadhani unamkumbuka yule aliyewai kufanya kazi klabuni Chelsea katika majukumu ya kufanya usajili, Michael Emenalo, unamkumbuka? alipigwa vita sana na mashabiki wengi wa Chelsea mwisho wa siku akaamua kuandika barua ya kujiuzulu kwenye nafasi hiyo. Naamini ushamkumbuka!

Sasa jamaa huyo mara baada ya kuondoka Chelsea mwaka jana alijiunga na klabu ya AS Monaco ya nchini Ufaransa ambapo huko alipewa majukumu hayohayo ya kushughulika na maswala ya usajili.

Taarifa zinaeleza, jamaa huyo mwenye asili ya Afrika ameanza kumfuatilia nyota wa klabu ya CSKA Moscow, Aleksander Golovin ambaye amekuwa akihusishwa mara kadhaa kutakiwa na Chelsea.

Golovin amekuwa msaada mkubwa kwa timu yake ya taifa ya Urusi kwenye michuano ya Kombe la Dunia na hivyo kuzivutia klabu kadhaa barani Ulaya.

Kumbuka Emenalo ameshafanikiwa kumsaini nyota kinda wa Chelsea, Panzo ambaye amejiunga na AS Monaco siku kadhaa zilizopita.

Je hii ni vita ya Emenalo dhidi ya Chelsea?

Pia unaweza kupata habari fupi kuhusu klabu ya Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905

No comments:

Post a Comment