Jioni ya jana kulichezwa mchezo wa fainali ya michuano ya Kombe la Dunia kati ya Ufaransa dhidi ya Croatia, mchezo uliomalizika kwa Ufaransa kuibuka mabingwa wapya wa michuano hiyo mara baada ya kupata ushindi wa mabao 4-2.
Lakini hiyo ilikuwa ni jambo zuri kwa nyota wa Chelsea, N'Golo Kante na Olivier Giroud ambao walikuwa sehemu ya timu hiyo kutwaa ubingwa huo wa pili kwa taifa hilo.
Lakini nadhani unakumbuka Kante hakuwa kwenye kiwango kizuri ambacho wengi walimzoea nacho.
Unajua sababu ni nini iliyomfanya nyota huyo kucheza chini ya kiwango mpaka akafanyiwa mabadiliko katika dakika ya 55? ambapo nafasi yake ilichukuliwa na Steven N'zozi?
Gazeti la Metro limeripoti kwamba sababu iliyomfanya Kante kucheza chini ya kiwango mpaka akatolewa ni kutokana na ugonjwa wa tumbo uliompata ghafla wakati wa mchezo huo. Inaelezwa alipata ugonjwa wa kuumwa tumbo na kumsababisha kutokuwa na hali nzuri wakati mchezo ukiwa unaendelea. Ugonjwa huo husababishwa na bakteria unaotajwa kuitwa 'Gastroenteritis'
Lakini hilo halikuizuia timu yake ya Ufaransa kutwaa ubingwa huo.
Hongera kwake na kwa nyota wenzake wa Ufaransa.
No comments:
Post a Comment