Klabu ya Chelsea inaweza kumpoteza nyota wake, Willian Borges ambaye inaelezwa anataka kujiunga na klabu ya Barcelona ambayo mpaka sasa inaendelea kuishawishi klabu ya Chelsea iweze kuwauzia nyota huyo raia wa Brazil.
Lakini mbrazil mwenzake klabuni Chelsea, David Luiz anaamini nyota huyo hatoweza kuondoka Chelsea kutokana na mapenzi aliyokuwa nayo kwa klabu hiyo yenye makazi yake huko jijini London nchini Uingereza.
"Willian hawezi kuondoka Chelsea, kwasababu anapenda kucheza hapa" alisema David Luiz ambaye jana aliiongoza Chelsea kupata ushindi wa goli 1- 0 dhidi ya Perth Glory huko nchini Australia.
Willian kwasasa yupo mapumzikoni mara baada ya kumalizika kwa michuano ya Kombe la Dunia ambapo yeye alishiriki kwa timu ya Brazil.
No comments:
Post a Comment