Hazard agombania tunzo dhidi ya Ronaldo na Messi - Darajani 1905

Hazard agombania tunzo dhidi ya Ronaldo na Messi

Share This

Mwezi May mwaka huu aliisaidia klabu ya Chelsea kubeba taji pekee msimu huu, taji la Kombe la FA katika mchezo wa fainali dhidi ya Manchester united huku mwenyewe akifunga goli pekee katika mchezo huo uliokuwa mchezo wa mwisho kwa kocha Antonio Conte kama kocha wa klabu hiyo.

Mwezi huu, mwezi Julai akaisaidia timu yake ya taifa kutwaa ushindi wa nafasi ya tatu kwenye michuano ya Kombe la Dunia huku akiichezea timu yake ya Ubelgiji michezo mitano na kufanikiwa kushinda tunzo ya mchezaji bora wa mchezo (man of the match) katika michezo minne na kusababisha kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa pili kwenye mashindano hayo akiwa nyuma ya Luca Modric aliyefanikiwa kufika fainali ya michuano hiyo.

Ni Eden Hazard, nyota huyo mwenye miaka 27 amefanikiwa kuingia kwenye orodha ya wachezaji 10 wanaowania tunzo ya mchezaji bora wa kiume kwa mwaka 2018 (FIFA Men's Best Player 2018).

Orodha kamili;
🔹Christiano Ronaldo
🔹Kevin De Bruyne
🔹Antoine Griezmann
🤙➡Eden Hazard
🔹Harry Kane
🔹Kylian Mbappe
🔹Lionel Messi
🔹Luka Modric
🔹Mohamed Salah
🔹 Raphael Varane

No comments:

Post a Comment