Chelsea kumpa kinda mwengine mkataba mpya - Darajani 1905

Chelsea kumpa kinda mwengine mkataba mpya

Share This

Katika mchezo wa jana aliingia kama mchezaji wa akiba na kucheza kwa dakika kadhaa huku ukiwa msimu wake mwengine akirejea kama mchezaji wa Chelsea katika kikosi cha wakubwa akitoka kwa mkopo alioutumikia akiwa klabuni Swansea ambako huko alienda kutokana na uwezo aliounyesha kwenye kikosi cha akademi ya Chelsea lakini sasa anaonekana kutumainiwa na kocha mpya klabuni hapo, Maurizio Sarri.

Eeh ndiyo hivyo, nyota kinda wa kikosi cha Chelsea, Tammy Abraham amepewa ofa ya kusaini mkataba mpya klabuni Chelsea huku ofa hiyo ikija mwaka mmoja toka aliposaini mkataba mpya ambao ulikuwa unamfanya apokee mshahara wa paundi 50,000.

Taarifa au ripoti zilizopo zinadai Chelsea imempa ofa ya mkataba wa miaka mitano na mshahara wa paundi 70,000 mshambuliaji huyo ambaye ni raia wa Uingereza.

Lakini pia akiahidiwa kupewa nafasi kwenye kikosi cha wakubwa ambacho msimu huu kipo chini ya kocha Maurizio Sarri ambaye inaonekana ana mahusiano mazuri na wachezaji vijana.

wakati huohuo, kumekuwa na taarifa zinazoaminika kwamba Chelsea inajiandaa kumpa mkataba mpya kinda mwengine, Callum Hudson-Odoi ambaye ana miaka 17 huku akionyesha kiwango kikubwa toka alipopewa nafasi kwa mara ya kwanza na kocha aliyeondoka klabuni hapo, Antonio Conte.

No comments:

Post a Comment