Fabregas afunga ndoa, huku N'Golo Kante akiibuka kituko - Darajani 1905

Fabregas afunga ndoa, huku N'Golo Kante akiibuka kituko

Share This

Juzi ilikuwa ni siku ya kwanza kwa Chelsea kucheza mchezo wake wa kwanza wa kirafiki wa kujiandaa na msimu mpya ambapo Chelsea ilisafiri mpaka nchinu Australia na kucheza dhidi ya Perth Glory huku Chelsea ikipata ushindi wa bao 1-0.

Ulikuwa ni mchezo wa kwanza kwa kocha mpya wa klabu hiyo, Maurizio Sarri lakini pia ulikuwa mchezo wa kwanza kwake huku akimtumia kiungo Cesc Fabregas kama nahodha huku nahodha mkuu wa Chelsea, Gary Cahill akiwa mapumzikoni kutokana na kushiriki michuano ya Kombe la Dunia.

Mara baada ya klabu hiyo kurejea nchini Uingereza ikaanza safari kwa baadhi ya nyota wa Chelsea ambapo walipewa ruhusa na kocha Maurizio Sarri ya kuhudhuria harusi ya kiungo na kaimu nahodha wa klabu hiyo, Cesc Fabregas ambapo alikuwa na harusi yake iliyofanyika huko nchini Hispania kwenye visiwa vya starehe vya Ibiza.

Bila shaka Fabregas hakusafiri pamoja na klabu kurejea nchini Uingereza na badala yake alifika kwenye visiwa hivyo ambako huko aliandaa shughuli ya kusherehekea harusi yake ambayo hakuifanya mara baada ya kufunga ndoa na mkewe Danielle Semaan mwezi May mwaka huu hivyo kuamua kuifanya usiku wa jumanne ya jana.

Harusi hiyo ilihudhuriwa na nyota wengi ambao ameshirikiana nao kwenye klabu za Arsenal, Barcelona na Chelsea huku baadhi ya nyota wa Chelsea walioshiriki ni pamoja na mchezaji wa zamani John Terry akihudhuria pamoja na mke wake, Marcos Alonso na mchumba wake, Ethan Ampadu, Ross Barkley, Davide Zappacosta na N'Golo Kante ambaye alifika akivaa shati la mikono mirefu rangi nyeupe na kaptula nyeusi akiwa kama ndiye gumzo kutokana na mavazi yake.

Fabregas na mkewe huyo wana watoto wanne..

No comments:

Post a Comment