Nyota 3 ambao wanakaribia kutua Chelsea - Darajani 1905

Nyota 3 ambao wanakaribia kutua Chelsea

Share This

Klabu ya Chelsea imefanikiwa kukamilisha usajili wa mchezaji mmoja tu mpaka sasa hivi, ambaye ni nyota aliyesajiliwa akitokea klabu ya Napoli kwa dau linalotajwa kufikia paundi milioni 57, Jorginho Frello, lakini je usajili wa nyota huyo mmoja unatosha kuifanya Chelsea iwe ya kiushindani zaidi haswa kutokana na ujio wa kocha mwenye falsafa mpya klabuni hapo, Maurizio Sarri. Sasa hapo hakuna jibu la moja kwa moja kama Jorginho anatosha au hatoshi.

Lakini tetesi zilizopo mpaka sasa ambazo zimekuwa zikipewa nafasi kukamilika pale klabuni Chelsea au kama sio kukamilika basi inapewa nafasi kubwa ni hii nayokuletea.

Danielle Rugani
Kutoka Juventus, mlinzi raia wa Italia anatajwa kufikia makubaliano binafsi ya kutua klabuni Chelsea huku ikielezwa amepewa ofa ya mshahara wa euro milioni 5 kwa mwaka tofauti na mshahara wa euro milioni 3 anaolipwa kwasasa huko Turin. Huyu ana nafasi kubwa ya kutua Chelsea.

Leon Bailey
Kutoka klabu moja huko nchini Ujerumani kwenye ligi kuu maarufu kama Bundesliga, klabu ya Bayer Leverkusen inaweza kupokea fungu nono kutoka Chelsea ili kumuuza nyota huyu raia wa Jamaica. Ingawa wengi wanachukulia kama usajili huu umeibuka ghafla lakini kama haujui nyota huyu ameanza kufukuziwa na Chelsea toka dirisha kubwa la usajili la mwaka uliopita. Moja ya picha zake alionekana akiwa na jezi za Chelsea pindi akiwa bado hajafikia hapa alipo kwasasa iliibua matumaini makubwa lakini pia kama haujui mara baada ya kumalizika kwa msimu uliomalizika nyota huyu alipiga picha akionekana nchini Uingereza kwenye jiji la London ambapo ilidhaniwa amefika huko ili kukutana na uongozi wa Chelsea. Ingawa anahusishwa pia kutakiwa na As Roma lakini naamini atachagua kutua Chelsea haswa kutokana na kujua kwake kwamba winga Willian Borges umri wake umeenda kwa hiyo ana muda mfupi wa kuwa juu.

Gonzalo Higuain
Kutua kwa Cristiano Ronaldo klabuni Juventus kunamaanisha nafasi finyu kwa Higuain kupata namba kikosini hapo na ukiangalia alikuwa na maisha mazuri alipokuwa chini ya kocha Sarri klabuni Napoli basi hii itakuwa na ushawishi mkubwa kwake kuamua kutua Chelsea.

Kwa leo naishia hapa...

No comments:

Post a Comment