Robert njiani kutua Chelsea - Darajani 1905

Robert njiani kutua Chelsea

Share This

Miaka 38 iliyopita kwenye kitongoji cha Chartesy huko jijini London kinachopatikana maili 10 kutoka ulipo uwanja wa mazoezi wa Chelsea maarufu kama Cobham alizaliwa mlinda mlango mkongwe raia wa Uingereza, Robert Green ambaye kwasasa anahusishwa kutua Chelsea.

Nyota huyo wa zamani ambaye aliwai kutamba vyema na klabu za Norwich na West Ham anaweza akakamilisha uhamisho wake wa kujiunga na wababe hao wa London muda wowote kuanzia sasa haswa kutokana na taarifa zinazoeleza kwamba amefanyiwa vipimo hii leo hii leo.

Green anatua Chelsea akiwa kama mchezaji huru kutokana na kumaliza mkataba wake na klabu ya Huddersfield united ambayo alijiunga nayo msimu uliopita huku asiichezee mchezo wowote. Anajiunga Chelsea kama mlinda mlango nambari tatu kutokana na makipa Jamal Blackman kujiunga na Leeds united kwa mkopo na Eduardo kujiunga na Vittese kwa mkopo.

No comments:

Post a Comment