Msikie Leroy Sane alichokisema kuhusu Chelsea - Darajani 1905

Msikie Leroy Sane alichokisema kuhusu Chelsea

Share This

Chelsea itacheza dhidi ya Manchester city katika mchezo wa Ngao ya Hisani siku ya tarehe 5-Agosti mwaka huu huko jijini London kwenye uwanja wa Wembley.

Mchezo huo utamaanisha kufunguliwa rasmi kwa michuano ya ligi kuu Uingereza na kombe la FA ambalo Chelsea ndiye bingwa huku Manchester city akiwa anaushikilia ubingwa wa ligi kuu.

Kuelekea msimu mpya wa 2018-2019, mchezaji wa Manchester city, Leroy Sane ametoa neno alipoulizwa anadhani ni klabu gani itakuwa changamoto katika kuwania ubingwa huo wa ligi kuu Uingereza ambapo nyota huyo raia wa Ujerumani alisema anadhani Chelsea itaipa changamoto sana klabu yake.

"Chelsea imempata kocha mpya. Kocha ambaye tulikuwa tunalihusudu aina ya soka lake na hata tulivyocheza dhidi yao tulipata tabu sana. Ingawa wachezaji itawachukua muda kulizoea soka lake lakini naamini watakuwa imara zaidi. Nafikiri Chelsea itatupa tabu sana msimu ujao" alisema nyota huyo ambaye msimu uliopita aliibuka mchezaji bora chipukizi.

No comments:

Post a Comment