Golovin kutua Chelsea? mapya yaibuka - Darajani 1905

Golovin kutua Chelsea? mapya yaibuka

Share This
Chanzo kimoja kinachoaminika kimeripoti kwamba nyota wa CSKA Moscow, Aleksandr Golovin amechagua kujiunga na AS Monaco huku akikataa kutua Chelsea.
Chelsea na AS Monaco zote zimekuwa zikitajwa kumfukuzia nyota huyo anayecheza nafasi ya kiungo.
Kama taarifa hizi zina ukweli basi nadhani Chelsea imemkosa nyota huyu raia wa Urusi kutokana na Chelsea kumnasa Jorginho Frello ambapo hii inapunguza uwezekano wa Golovin kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza. Kwasasa Chelsea ina viungo ambao ni Jorgingo, Cesc Fabregas, N'Golo Kante, Tiemoue Bakayoko, Danny Drinkwater na Ross Barkley

No comments:

Post a Comment