Rasmi; Green ni wa Chelsea - Darajani 1905

Hatimaye kocha Maurizio Sarri anafanikiwa kuongeza nyota mwengine klabuni Chelsea mara baada ya siku kadhaa kukamilisha uhamisho wa kwanza kwa kumsajili nyota Jorginho Frello aliyetoka nae klabuni Napoli huko nchini Italia.

Robert Green amekamilisha uhamisho wake wa mwaka mmoja akitua klabuni Chelsea kama mlinda mlango nambari tatu akiziba pengo la Eduardo aliyejiunga na klabu ya Vittese kwa mkopo akitokea Chelsea.

Robert Green mwenye miaka 38 amekamilisha usajili huo ambao mwenyewe anaamini umekuja wakati sahihi na mwafaka kwake na usisahau hii ndio klabu kubwa ya kwanza kwake kuichezea klabu kubwa inayoshiriki michuano ya Ulaya ambapo kabla alitamba vizuri akiwa na klabu za Norwich na West Ham.

Chelsea haijatumia dau lolote kumnasa nyota huyu kutokana na kutokuwa na mkataba na klabu yoyote huku msimu uliopita alitumika akiwa mlinda mlango wa klabu ya Huddersfield ambayo hakuichezea mchezo hata mmoja na alimaliza nayo mkataba mwishoni mwa msimu uliomalizika.

No comments:

Post a Comment