Morata akubali kuondoka Chelsea, klabu yahitaji donge nono ili kumuuza - Darajani 1905

Morata akubali kuondoka Chelsea, klabu yahitaji donge nono ili kumuuza

Share This

Nyota na mshambuliaji raia wa Hispania, Alvaro Morata amekubali kujiunga na klabu ya AC Milan inayoshiriki ligi kuu nchini Italia.

Nyota huyo ambaye ametua Chelsea katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi anatajwa kukubali ofa ya kujiunga na wababe hao wa jiji la Milan huko nchini Italia huku Chelsea ikitaka dau la paundi milioni 62 ili kumuuza mshambuliaji huyo mwenye miaka 25.

Morata amekuwa akihusishwa mara kadhaa kutaka kujiunga na klabu ya Juventus ya nchini Italia lakini klabu hiyo kufanikiwa kwake kumnasa Cristiano Ronaldo kunatajwa kufifisha jitihada za nyota huyo kurejea klabuni huko ambapo aliwai kutamba kabla ya kurejea Real Madrid na baadae Chelsea kumnasa kwa dau la paundi milioni 60.

No comments:

Post a Comment