Kama Hazard akiondoka Chelsea, basi huyu ndiye mrithi wake - Darajani 1905

Kama Hazard akiondoka Chelsea, basi huyu ndiye mrithi wake

Share This

Klabu ya Chelsea inahaha kumbakiza nyota Eden Hazard ambaye inaaminika anataka kujiunga na klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania ambapo huko inaaminika anahitajika ili kuziba pengo la mreno, Cristiano Ronaldo aliyetimkia klabu ya Juventus ya nchini Italia.

Lakini kama nyota huyo ambaye amebakiza mkataba wa miaka miwili klabuni Chelsea ataondoka klabuni hapo basi inaripotiwa kwamba Chelsea itamnasa Wilfred Zaha kutoka Crystal Palace.

Mwandishi mmoja wa tovuti ya habari za michezo ya talkSPORT amesema klabu ya Chelsea imepanga kumtumia Wilfred Zaha kama nyota mbadala wa Eden Hazard endapo mbelgiji huyo atafikia maamuzi ya kuondoka Chelsea

No comments:

Post a Comment