Green hataki kupoteza muda, aanza kwa mbwembwe kibao - Darajani 1905

Green hataki kupoteza muda, aanza kwa mbwembwe kibao

Share This

Asubuhi ya leo klabu ya Chelsea imekamilisha rasmi usajili wa nyota mlinda mlango Robert Green ambaye amesajiliwa akiwa kama mlinda mlango chaguo la tatu nyuma ya makipa Thibaut Courtois na Willy Caballero.

Mara baada ya kukamilisha usajili huo, mlinda mlango huyo hakutaka kupoteza muda na badala yake akaungana na nyota wengine klabuni hapo katika mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa kirafiki unaokuja dhidi ya Inter Milan utakaochezwa tarehe 28-Julai huko nchini Ufaransa.

Alipofika mazoezini hapo akakutana na nyota wenzake wa Chelsea akiwemo mlinda mlango nambari mbili, Willy Caballero ambaye amerejea mazoezi siku chache zilizopita akitokea kwenye mapumziko aliyopewa kutokana na kumalizika kwa michuano ya Kombe la Dunia.
Nyota huyo mwenye miaka 38 amesajiliwa kwa usajili wa bure mara baada ya kumaliza mkataba wake aliokuwa nao na klabu ya Huddersfield.

No comments:

Post a Comment