Rasmi; Maddox atimka Chelsea - Darajani 1905

Klabu ya Chelsea inazidi kuongeza idadi ya wachezaji wake ambao wametolewa kwa mkopo mara baada ya siku ya leo kumtoa kwa mkopo nyota mwengine mwenye miaka 19, Jacob Maddox ambaye anatimiza idadi ya wachezaji 20 ya wachezaji waliotolewa kwa mkopo.

Maddox amenkamilisha uhamisho aa kujiunga kwa mkopo na klabu ya Cheltenham Town ambako huko ataichezea kwa mkopo mpaka mwishoni mwa msimu ujao.

Maddox alijunga na Chelsea akiwa na miaka 14 huku kwasasa anaichezea klabu ya vijana ya timu ya taifa ya Uingereza chini ya miaka 20 huku akifanikiwa kushinda mataji kadhaa akiwa na klabu za vijana za Chelsea ambayo ni pamoja na makombe mawili ya FA kwa vijana na klabu bingwa barani Ulaya kwa vijana hiyo ikiwa ni mwaka 2017.

No comments:

Post a Comment