Courtois amesaini Chelsea? kwanini Madrid wameachana na Hazard? majibu yote yapo hapa - Darajani 1905

Courtois amesaini Chelsea? kwanini Madrid wameachana na Hazard? majibu yote yapo hapa

Share This

Nyota wawili raia wa Belgiji klabuni Chelsea, Thibaut Courtois ambaye ni mlinda mlango na Eden Hazard wamekuwa wakihusishwa kuhusu kuondoka klabuni hapo huku klabu inayotajwa kuwafukuzia ikiwa ni klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania.

Thibaut Courtois anahusishwa kutakiwa na klabu hiyo ambayo inataka kipa atakayekuwa na uwezo mkubwa kuliko kipa wao wa sasa, Keylor Navas huku Hazard akihusishwa ili kuziba pengo la Cristiano Ronaldo aliyejiunga na Juventus kwa usajili wa kushtukiza uliogharimu euro milioni 100.

Kipi kilichojiri!
Mpaka sasa Thibaut Courtois yupo nchini Hispania ambako huko alifika ili kujumuika na familia yake kama sehemu ya mapumziko yake, familia ambayo aliipata akiwa kwa mkopo klabuni Atletico Madrid, taarifa za mwisho zimeripoti kwamba nyota huyo amefikia makubaliano binafsi ili ajiunge na klabu hiyo. Ingawa bado ni tetesi.

Kwa upande wa Hazard taarifa zinasema klabu ya Real Madrid imeachana na mpango wake wa kumsajili nyota huyo kutokana na dau lililotajwa na Chelsea kama thamani ya winga huyo nasasa imeamishia nguvu zake kwa mshambuliaji raia wa Uruguay, Edinson Cavani. Chelsea ilitaka euro milioni 200 ili imuuze nyota huyo.

No comments:

Post a Comment