Chanzo cha habari kinachoaminika barani Ulaya kimetoa ripoti kwamba klabu ya Chelsea imefikia makubaliano na klabu ya CSKA Moscow juu ya kumsajili nyota wa klabu hiyo, Aleksander Golovin.
Taarifa hizo zinaeleza nyota huyo yupo tayari kufanyiwa vipimo vya afya ili kujiunga na Chelsea ambayo nayo imekubaliana nae mahitaji binafsi.
Chelsea inatajwa kuzipiku klabu za Juventus na AS Monaco ambazo nazo zimetajwa kumfukuzia. Paundi milioni 25 ndilo dau linalotajwa.
No comments:
Post a Comment