Kama kocha Maurizio Sarri akilifanya hili, basi Gary Cahill ataondoka - Darajani 1905

Kama kocha Maurizio Sarri akilifanya hili, basi Gary Cahill ataondoka

Share This

Chelsea inatajwa kumfukuzia mlinzi wa klabu ya Juventus, Danielle Rugani mwenye miaka 23 lakini usajili huo unatajwa kutokuwa mzuri kwa upande wa nahodha wa Chelsea, Gary Cahill.

Taarifa zilizopo zinadai kutua kwa Rugani klabuni Chelsea kutamaanisha ufinyu wa kupata nafasi kwa nahodha huyo alisajiliwa na Chelsea akitokea klabu ya Bolton Wanderers mwaka

Nyota huyo raia wa Uingereza anatajwa kupanga kuondoka klabuni hapo endapo Danielle Rugani akitua klabuni hapo haswa kutokana na ufinyu wa kupata nafasi kwenye kikosi cha Chelsea.

Rugani anatajwa kukaribia kutua Chelsea huku dau la paundi 35 likitajwa kuhusika kwenye usajili ambao unatajwa kushinikizwa na kocha Maurizio Sarri.

No comments:

Post a Comment