Siku ya tarehe 13-Julai, ijumaa iliyopita klabu ya Chelsea ilithibitisha rasmi kuachana na kocha wake Antonio Conte aliyeifundisha klabu hiyo kwa misimu miwili toka atue klabuni hapo mwaka 2016 akitokea timu ya taifa ya Italia ambapo huko aliiongoza kama kocha.
Lakini sasa kocha huyo hayupo tena Chelsea na nafasi yake imechukuliwa na kocha muitaliano mwenzake, Maurizio Sarri.
Lakini kwa misimu miwili ambayo kocha huyo ameiongoza Chelsea kushinda mataji mawili ya ligi kuu Uingereza na Kombe la FA haijamfanya aondoke hivihivi bila kuacha ujumbe kwa muda wote aliopo Chelsea.
Kocha huyo ameandika barua inayosomeka;
"Napenda kuwashukuru marafiki zangu wote wa Chelsea kwa yote waliyoyafanya kwa misimu miwili yaliyotusaidia kushinda Ligi kuu Uingereza na Kombe la FA tukiwa pamoja."
"Kwa wachezaji ambao vipaji vyao na kujituma kwao kulikosaidia mafanikio yetu, nawashukuru kwa kila kitu maana imekuwa ni ufahari na jambo zuri kufanya nao kazi kila siku."
"Kwa viongozi na benchi la ufundi ambao walifanya kazi kwa uwezo mkubwa na kujidhatiti ni lazima niseme asante kwa uwezo wao na kwa walivyoonyesha ubora wao"
"Nimefurahia maisha yangu ya Uingereza na London na nataka niwashukuru mashabiki wote wa Chelsea ambao walinipa ushirikiano kwangu na kwa familia yangu. Lilikuwa ni jambo zuri kwangu kuungana kihisia na kuwa tayari kupambana na mashabiki wote wa Chelsea kwa misimu yote miwili ambayo ni ngumu kuisahau, siku zote nitaendelea kuwakumbuka mashabiki wa Chelsea na daima wapo moyoni mwangu"
"Natumaini Chelsea itaendelea kuwa na mafanikio na nawatakia heri kila mmoja kwa msimu ujao. Nimefanikiwa kutengeneza matukio mengi ya kumbukumbu nikiwa Chelsea ambayo nitayatumia katika changamoto zangu nyengine"
No comments:
Post a Comment