Chelsea imekuwa ikimfukuzia nyota raia wa Urusi anayeichezea klabu ya CSKA Moscow, Aleksander Golovin ambaye ameng'aa vizuri kwenye michuano ya Kombe la Dunia akiwa na timu yake ya taifa ambayo iliishia katika hatua ya robo fainali.
Kumeenea taarifa nyingi kuhusu Chelsea kukaribia kumnasa nyota huyo huku ikizishinda klabu za Juventus na AS Monaco ambazo zote zimekuwa zikitajwa kumfukuzia.
Lakini rais wa klabu yake ya CSKA Moscow amefunguka kuhusu usajili wa nyota huyo ambapo alipoulizwa kuhusu Chelsea kumfukuzia nyota huyo alisema "Chelsea? sina taarifa kamili kuhusu hilo, lakini nadhani kwenye kuamua klabu ya atakayoichezea kutafanyika mara baada ya siku chache zijazo."
Alipoulizwa kuhusu kumruhusu nyota huyo kuondoka klabuni hapo, rais huyo alisema "Sidhani kama litakuwa jambo sahihi kwetu kumzuia"
Lakini vipi kuhusu klabu ya AS Monaco kuhusishwa kumfukuzia nyota huyo, alisema "Moja ya viongozi wa klabu ya Monaco nilifanya nae mkutano mdogo na alinieleza nia ya kumtaka nyota huyo"
No comments:
Post a Comment