Bila shaka utakubaliana nami nkisema aling'aa sana kwenye mchezo wa marudiano wa Kombe la FA dhidi ya Norwich, mchezo wa ligi kuu dhidi ya Liverpool wakati Chelsea ilipoibamiza Liverpool bao 1-0 na mchezo wa fainali ya Kombe la FA dhidi ya Man utd. Huenda unakubaliana nami au unanipinga lakini kwangu naamini uwezo mkubwa alioonyesha kwenye mchezo huo ulionekana.Na usisahau alichaguliwa kuwa nyota wa mchezo kwenye mchezo wa marudiano wa kombe la FA dhidi ya Norwich.
Nirudi kwenye habari, huyo ni nyota kiungo wa klabu ya Chelsea raia wa Ufaransa, Tiemoue Bakayoko anatajwa kufukuziwa kwa mkopo na klabu ya Sevilla ya nchini Hispania.
Bakayoko ambaye hakuwa na msimu mzuri katika msimu wake wa kwanza klabuni Chelsea akisajiliwa akitokea klabu ya AS Monaco ambako huko aliisaidia klabu hiyo kushinda ubingwa wa ligi kuu Ufaransa maarufu kama Ligue 1.
No comments:
Post a Comment