Niite ni mchana au jioni? nadhani ni jioni kwa nchi za Afrika Mashariki ambapo mishale ya saa 4:00 (saa 16:00) ambapo huko nchini Uingereza itakuwa saa 2:00 mchana (saa 14:00) hii leo kutafanyika mkutano wa kwanza kwa waandishi wa habari ambapo watamhoji kocha mpya wa Chelsea, Maurizio Sarri.
Taarifa zilizopo zinaeleza kocha huyo ambaye ameanza mazoezi rasmi na wachezaji waliorejea klabuni Chelsea ambao hawakushiriki michuano ya Kombe la Dunia atafanya mkutano huo na waandishi wa habari ambao watapata fursa ya kufanyiwa mahojiano na kuulizwa maswali na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza toka atangazwe kuwa kocha mpya wa Chelsea.
Darajani 1905 itakuletea kila linalojiri kuhusu mkutano huo.
No comments:
Post a Comment