Unamkumbuka yule nyota mfupi raia wa Uingereza aliyewai kutamba klabuni Chelsea, anaitwa Wright-Phillips, ushamkumbuka?
Siku kama ya leo yaani tarehe 18-Julai mwaka 2005 ndio alisajiliwa na Chelsea akitokea klabu ya Manchester city. Jina lake kamili ni Shaun Cameron Wright-Phillips ambaye alishinda mataji karibu yote ya ndani ya Uingereza namaanisha ligi kuu Uingereza msimu wa 2005-2006, Kombe la FA, Ngao ya Hisani lakini alishindwa kubeba kombe la ligi ambalo waliishia katika hatua ya fainali.
Leo inatimia miaka 13 toka nyota huyo asajiliwe na Chelsea akiitumikia kwa mafanikio makubwa lakini akisajiliwa kwa paundi milioni 21 lakini mwaka 2008 akauzwa na kurejea Manchester city kabla ya baadae kuuzwa tena kwenda QPR na baadae akatimkia huko Marekani.
Kwa sasa anacheza kwenye klabu ya Phoenix ya nchini Marekani ambayo moja wa wamiliki wa klabu hiyo ni gwiji wa Chelsea, Didier Drogba.
Jambo usilolijua kuhusu nyota huyu, alichukuliwa kwenye kituo cha kulelea watoto wasio na wazazi au wazazi wao hawana uwezo wameamua kuwapeleka kwenye vituo maalumu (kuwa adopted) na gwiji wa soka Ian Wright ambaye aliwai kutamba na klabu ya Arsenal ambapo gwiji huyo alimchukua mtoto huyo akiwa na miaka mitatu.
Unamkumbuka kwa lipi? sio kwa ule ukiberenge wake? namaanisha uwezo wake mkubwa wa kukimbia...
No comments:
Post a Comment