Sarri aanza kushughulika na Alisson - Darajani 1905

Sarri aanza kushughulika na Alisson

Share This

Taarifa zilizoripotiwa na chombo kimoja cha habari zinasema kocha wa Chelsea, Maurizio Sarri amefanya mawasiliano na mlinda mlango wa As Roma, Alisson Becker akijaribu kumshawishi ili kipa huyo atue Chelsea.

Alisson anatajwa kwa karibu kutakiwa na klabu ya Liverpool huku Chelsea ikitajwa kumuwania pia ili kuziba pengo la mlinda mlango nambari moja wa Chelsea, Thibaut Courtois ambaye anatajwa kukaribia kutua Real Madrid.

Chelsea imemuandalia Alisson mshahara wa euro milioni 6 kwa mwaka huku As Roma wakitaka euro milioni 70 ili kumuuza kipa huyo raia wa Brazil.

No comments:

Post a Comment