Alichokizungumza kocha Maurizio Sarri kwenye mkutano wake hii leo (18-Julai-2018) - Darajani 1905

Alichokizungumza kocha Maurizio Sarri kwenye mkutano wake hii leo (18-Julai-2018)

Share This

Kocha wa Chelsea, Maurizio Sarri amefanya mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari hii leo ukiwa ni mkutano wake wa kwanza toka atambulishwe kuwa kocha mpya wa Chelsea.

Hapa ninakuletea baadhi ya mambo aliyoyazungumzia katika mkutano huo ambapo alianza kwa kusema anafurahi kuwa klabuni Chelsea.

Alipoulizwa kuhusu uwezekano wa kuwabakisha nyota wa Chelsea, Thibaut Courtois na Eden Hazard ambao wanahusishwa kuondoka wakitakiwa na klabu ya Real Madrid, kocha huyo amesema "Tunapenda kubaki na kila mchezaji nyota. Naamini kila kocha au klabu inapenda kubaki na wachezaji wake bora lakini tutaangalia soko la usajili litakavyokuwa baada ya siku chache zijazo"

Alipoulizwa kuhusu maswala ya usajili klabuni hapo, kocha alisema "Najihisi mimi ni kocha ninayependa kucheza sana uwanjani sipo vizuri sana kuhusu maswala yote kwa ujumla. Huwa nina kawaida ya kuwatumia wale wachezaji waliopo. Mimi ni kocha ambaye sipendeleagi sana kushughulika na usajili"

Alipoulizwa kuhusu kocha wa Manchester city, Pep Guardiola ambaye amekuwa naye karibu, kocha Sarri alisema "Guardiola ni bingwa na ni mtu mwenye akili sana. Hakika kwenye msimu wake wa kwanza alikuwa na msimu mbaya lakini kufika alama 100 kwenye msimu wake wa pili ni jambo ambalo hakika linaonyesha kwa kiasi gani alivyo na akili na ninahisi rekodi yake ni ngumu kufikiwa"

Alipoulizwa kuhusu klabu ya Chelsea alijibu kwa kusema "Siwezi kuwabadilisha wachezaji 20 lakini ni lazima nishirikiane nao vizuri na kwenda nao sawa kisha tutaona kama tutabadilisha chochote kikosini kulingana na hali itakavyokuwa"

"Siwezi kutaja jina la mchezaji yoyote lakini nimeongea na klabu kwamba tunatakiwa kuongeza ubora haswa kwenye sehemu ya viungo wa kati ili kuendana na aina ya mchezo" alisema kocha huyo.

Una maoni gani katika hili? tafadhali acha maoni yako chini...

No comments:

Post a Comment