Klabu ya Chelsea imeanza safari hii leo ili kuelekea nchini Australia ambako huko itacheza mchezo mmoja wa kirafiki ambao utakuwa mchezo maalumu katika ufunguzi wa uwanja mpya wa Opta Stadium ambao unatumiwa na timu ya Perth Glory.
Chelsea itacheza mchezo huo wa kirafiki dhidi ya klabu hiyo ya Perth Glory siku ya tarehe 23-Julai ukiwa ni mchezo wa kwanza wa kirafiki na pia ukiwa mchezo wa kwanza kwa kocha mpya wa Chelsea, Maurizio Sarri.
Kocha huyo amechagua kikosi cha wachezaji 25 watakaocheza michezo ya kirafiki ya kujiandaa na msimu mpya wa 2018-2019.
Kikosi hicho ni;
Marcin Bulka, Jared Thompson, Bradley Collins, David Luiz, Ethan, Ampadu, Fikayo Tomori, Michael Hector, Tomas Kalas, Marcos Alonso, Emerson, Davide Zappacosta, Ola Aina, Cesc Fabregas, Danny Drinkwater, Tiemoue Bakayoko, Ross Barkley, Mario Pasalic, Jorginho, Kasey Palmer, Pedro, Lucas Piazon, Charly Musonda, Callum Hudson-Odoi, Alvaro Morata na Tammy Abraham
No comments:
Post a Comment