Bado mabadiliko yanaendelea kufanyika klabuni Chelsea toka kufika kwa kocha Maurizio Sarri ambaye mpaka leo itakuwa amebakiza siku moja ili kukamilisha wiki moja tangu alipotambulishwa rasmi kwamba atakuwa kocha mpya wa Chelsea akichukua nafasi ya kocha muitaliano mwenzake, Antonio Conte.
Hatimaye kocha huyo amekamilisha taarifa nyengine kwa kumchagua aliyewai kuwa nyota wa Chelsea, Gianfranco Zola kuwa moja ya makocha wasaidizi kwenye benchi la ufundi la Chelsea.
Kumekuwa kuna fununu za muda mrefu juu ya gwiji huyo kuweza kushika madaraka hayo ambapo hilo limeonekana kutimia hii leo ambapo gwiji huyo aliposafiri pamoja na wachezaji wa Chelsea kuelekea nchini Australia ambapo huko Chelsea itacheza mchezo wake wa kirafiki dhidi ya klabu ya Perth Glory.
Zola alipohojiwa juu ya kuchaguliwa kwake kwenye nafasi hiyo, gwiji huyo alisema amefurahishwa kuchaguliwa katika nafasi hiyo huku akiamini kazi hiyo ni ngumu lakini atajitahidi kufanya kazi kwa nguvu na kwa kujitoa kama alivyojitoa mwanzo akiwa kama mchezaji.
No comments:
Post a Comment