Klabu ya Chelsea imeanza safari ya kuelekea nchini Australia ambako huko itacheza mchezo wake mmoja wa kirafiki dhidi ya Perth Glory siku ya tarehe 23-Julai mwaka huu.
Safari hii ni inamaanisha sasa Chelsea inaanza kujiandaa kwa ajili ya msimu ujao wa 2018-2019.
Lakini nadhani wote tunafahamu kikosi kilichoanza mazoezi toka siku ya jumatatu iliyopita kilikuwa hakijawajumuisha wale nyota ambao walikuwepo kwenye michuano ya Kombe la Dunia ambapo ndani yake kulikuwa na walinda milango wawili wa Chelsea ambao ni Thibaut Courtois aliyeiongoza Ubelgiji na Willy Caballero aliyeiongoza timu ya Argentina, hiyo inamaanisha nini? hii inamaanisha kuondoka kwa kikosi cha Chelsea cha wachezaji 25 kwenda nchini Australia kimekwenda bila mlinda mlango nambari moja, Thibaut Courtois, mlinda mlango nambari mbili Willy Caballero na Eduardo ambaye mwenyewe ni mlinda mlango nambari tatu ambaye ametolewa kwa mkopo kwenye klabu ya Vitesse ya nchini Uholanzi.
Sasa je nani atakuwa mlinda mlango kwenye michezo hii ya kirafiki?
Darajani 1905 inakujuza kwamba kocha Maurizio Sarri amewachagua walinda milango watatu kutoka kwenye timu za akademi za vijana klabuni Chelsea.
Bladley Collins anaweza kutumika mlinda mlango nambari moja kwenye michezo hiyo ya kirafiki kutokana na umri wake wa miaka 21 lakini pia msimu uliopita alitolewa kwa mkopo, Marcin Bulka nae ni mlinda mlango mwenye kipaji cha hali ya juu huku akiwa na miaka 18 wakati kipa mwengine akiwa ni Thompson ambaye ana miaka 19 akiwa pia anaichezea klabu ya vijana ya Chelsea.
No comments:
Post a Comment