Maurizio Sarri kumtimua Kurt Zouma? - Darajani 1905

Maurizio Sarri kumtimua Kurt Zouma?

Share This

Klabu ya Chelsea ilimsajili akitokea klabu ya St. Etienne ya nchini kwao Ufaransa huku akionyesha uwezo mkubwa kabla ya kupata majeraha miaka miwili iliyopita ambayo yalimfanya kuwa nje kwa muda mrefu lakini baadae akarejeshwa na kupewa mkataba mpya wa miaka sita na ndipo Chelsea ikaamua imtoe kwa mkopo kwenye klabu ya Stoke city. Huyo ni mlinzi wa Chelsea, Kurt Happy Zouma.

Kwa fununu zilizopo zinadai nyota huyo anaweza kuondoka klabuni Chelsea huku sababu inayoonekana ni kuachwa kwenye kikosi cha wachezaji 25 ambao wamesafiri kuelekea nchini Australia ambako huko watacheza mchezo mmoja wa kirafiki. Tarehe 23-Julai.

Kuona wachezaji walioitwa kwenye kikosi hicho cha wachezaji 25, bonyeza hapa

No comments:

Post a Comment