Moja kati ya mambo ambayo mpaka sasa bado hayajapatiwa ufumbuzi pale klabuni Chelsea ni juu ya mmiliki wa klabu hiyo, Roman Abramovich kushindikana kupata kupata kibali cha kuendelea kuishi nchini Uingereza hali inayotajwa kusababisha kusimamishwa kwa mipango ya upanuzi wa uwanja wa Chelsea, Stamford Bridge lakini pia ikidhaniwa tajiri huyo anayeishi nchini Israel kwasasa kutaka kuiuza klabu hiyo.
Je kocha mpya klabuni hapo, Maurizio Sarri analichukulia vipi swala la mmiliki huyo kukosa kibali cha kuishi nchini Uingereza? hilo ni swali aliloulizwa kocha huyo mwenye miaka 59 hapo jana akiwa kwenye mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari toka alipotambulishwa rasmi kuwa kocha mpya wa Chelsea jumamosi iliyopita ya tarehe 14-Jumamosi.
"Nadhani swala la kibali ni swala la mtu binafsi, nami nina muda mfupi hapa siwezi kufika na kuongea na kumuuliza kuhusu maswala yake binafsi" alijibu kocha huyo ambaye jana alikiongoza kikosi cha wachezaji 25 kuelekea nchini Australia ambapo huko itacheza mchezo wake mmoja wa kirafiki wa kujiandaa na msimu wa 2018-2019.
Ujenzi na upanuzi wa uwanja wa Stamford Bridge unaokadiriwa kugharimu paundi bilioni 1 unatajwa kusimamishwa muda mfupi toka mmiliki huyo kumaliza kibali chake cha kuishi nchini Uingereza kilichoisha mwezi Aprili mwaka huu hali iliyomfanya kushindwa kuhudhuria mchezo wa fainali ya Kombe la FA kati ya Chelsea dhidi ya Manchester united uliochezwa mwezi May mwaka, huu mchezo uliomalizika kwa Chelsea kuibuka mabingwa.
No comments:
Post a Comment