Tajiri afunga safari kumfata Donnaruma - Darajani 1905

Tajiri afunga safari kumfata Donnaruma

Share This

Mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich amefika nchini Italia kwenye jiji la Milan ambapo inaelezwa amekutana na wakala wa mlinda mlango wa AC Milan, Gigi Donnaruma ili nyota huyo atue Chelsea.

Inaripotiwa mlinda mlango huyo anataka kuondoka klabuni hapo huku akidai kutaka kufanya kazi na kocha wa Chelsea, Maurizio Sarri.

Chelsea inaweza ikampoteza mlinda mlango wake nambari moja, Thibaut Courtois ambaye anahusishwa kutimkia Real Madrid.

No comments:

Post a Comment