Abramovich ampa masharti 3 kocha Maurizio Sarri - Darajani 1905

Abramovich ampa masharti 3 kocha Maurizio Sarri

Share This

Mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich amempa masharti kocha mpya wa klabu hiyo, Maurizio Sarri ambaye ametua klabuni Chelsea akitokea Napoli ya nchini Italia.

Masharti hayo ni;
1. Kutokuvaa fulana na suruali laini (track-suit) kwenye michezo ambayo Chelsea itakuwa uwanjani lakini pia kwenye mikutano ya waandishi wa habari akiwa kama kocha wa Chelsea huku akiamriwa kuvaa suti. Na hilo alilitimiza jana kwenye mkutano wake wa kwanza akiwa na waandishi wa habari ambapo alivaa suti tofauti na alivyozoea huko nchini Italia.
2. Kutokuvuta sigara wakati wa mapumziko na kutohusika kwenye matukio yasiyo ya kiuanasoka wakati hilo alikuwa akihusika nalo pindi alipokuwa nchini Italia ambapo huko amekuwa akivuta sigara na kupata kashfa mbaya.
3. Kupewa mtu atakayempa mafunzo ya kuendesha gari haswa kutokana na mfumo wa uendeshaji magari nchini Uingereza ikitofautiana na Italia alipotoka. Uingereza wanatumia mfumo wa kushoto wa uendeshaji wakati Italia wanatumia mfumo wa kulia.

No comments:

Post a Comment