Katika moja ya tovuti zinazoripoti habari za michezo huko barani Ulaya imeripoti kwamba baba wa winga na nyota wa Chelsea Eden Hazard ambaye anaitwa Thierry Hazard amezungumzia uhamisho wa mtoto wake ambaye alijiunga na Chelsea katika dirisha kubwa la usajili lililopita, Kylian Hazard.
Baba huyo alifanyiwa mahojiano na chombo kimoja cha habari na kusema mwanae huyo mwenye miaka 23 ataondoka Chelsea na kujiunga kwa mkopo na klabu ya nchini Hispania.
"Kylian ana mkataba wa miaka miwili na Chelsea lakini ataondoka kwa mkopo"
"Alifanyiwa vipimo na klabu ya VVV ya nchini Uholanzi lakini mambo hayakwenda sawa lakini sasa amepata nafasi huko nchini Hispania" alisema baba huyo wakati alipokuwa akifanyiwa mahojiano juu ya hatma ya nyota huyo.
Kylian alijiunga na Chelsea akitokea Ujpest uku akisaini mkataba wa miaka mitatu klabuni Chelsea, lakini.toka amefika amekuwa akitumika kwenye kikosi cha vijana wenye umri chini ya miaka 23 wa Chelsea ambapo hilo halionekani kumpendeza baba yake anayetamani nyota huyo atumike katika kikosi cha kwanza.
No comments:
Post a Comment