Mmiliki wa Klabu ya Chelsea Roman Abromovich ameiajiri benki ya New York Raine Group ikiwa ni maandalizi ya kuiuza Klabu hiyo, benki hiyo itahusika katika kuuza hisa au kumtafuta mmiliki mpya na benki hiyo imesema Klabu ya Chelsea inathamani ya paundi billion 2
Mapema mwaka huu (2018) Roman Abromovich alikataa kuiuza Klabu hiyo kwa tajiri mkubwa nchini Uingereza aitwaye Sir Jim Ratcliffe ambaye alikuwa tayari kutoa kiasi cha paundi billion 2.
Abramovich alikataa ofa hiyo kwasababu alikuwa alitaka kuiuza Chelsea kwa kiasi cha zaidi ya paundi billion 2. Na endapo dili hili litafanikiwa basi hii itakuwa ni rekodi ya Dunia kwa Klabu ya soka kuuzwa kwa paundi billion 2
Waajiriwa hao ambao ni Raine Group wanatarajia kutafuta wawekezaji nchini China, United States na Mashariki ya Kati.
No comments:
Post a Comment