Ligi kuu Uingereza; Habari muhimu na uchambuzi kuelekea Newcastle vs Chelsea - Darajani 1905

Ligi kuu Uingereza; Habari muhimu na uchambuzi kuelekea Newcastle vs Chelsea

Share This
Ni siku nyengine iliyobarikiwa na mwenyezi Mungu, shukrani kwake kwa kututanya tu wazima na wenye afya, tunawatakia pole na hali njema wazidi kuimarika na kupona haraka wale wote walio mahospitalini wanaouguza au kuuguza wagonjwa.

Siku ya leo ya tarehe 26-Agosti, klabu yetu pendwa ya Chelsea itakuwa uwanjani kucheza mchezo wake wa tatu wa ligi kuu Uingereza, ikicheza dhidi ya Newcastle united itakayokuwa nyumbani kwenye uwanja wake wa St. James' Park.

Kuelekea kwenye mchezo huo, hapa nakuletea habari muhimu unazopaswa kuzijua kuhusu mchezo huo.

Chelsea:
Kiungo wa Chelsea, Cesc Fabregas ataukosa mchezo wa leo kutokana na majeraha aliyoyapata katika mchezo wa kirafiki ambapo Chelsea ilimenyana dhidi ya Arsenal na hivyo kumfanya kukosa michezo miwili ya ligi kuu wakati Chelsea ilipomenyana dhidi ya Huddersfield Town na Arsenal.

Lakini leo kuna uwezekano wa Eden Hazard na Mateo Kovacic wakapata nafasi ya kuanza mara baada ya kocha Maurizio Sarri kusema anafikiri nyota hao wapo tayari kucheza kwa dakika 50 au 60. Kama unakumbuka vyema wawili hao walicheza kwa dakika 30 tu katika mchezo uliopita dhidi ya Arsenal.

Newcastle:
Kennedy Robert ataukosa mchezo huu kutokana na sheria za mchezaji wa mkopo kutoruhusiwa kucheza dhidi ya timu yake iliyomtoa kwa mkopo. Nyota huyo anacheza Newcastle kwa mkopo akitokea Chelsea. Nyota wengine watakaoukosa mchezo huu ni pamoja na Lejeune, Manquillo na Hayden.

Mwamuzi:
Paul Tierney ndiye mwamuzi katika mchezo wa leo. Mwamuzi huyo hajawai kuwa mwamuzi wakati Chelsea ilipokuwa uwanjani lakini kwa upande wa Newcastle, amekuwa mwamuzi katika michezo mitano, klabu hiyo imepata ushindi katika mchezo mmoja dhidi ya Barnsley mwaka 2016 huku ikipoteza michezo minne.

Mchezo uliopita:
Katika mchezo uliopita pindi klabu hizi zilipomenyana uliisha kwa Chelsea kupoteza kwa magoli 3-0 wakati Newcastle alipokuwa nyumbani msimu wa 2017-2018.

Uchambuzi;
Nafikiri kubwa linalowasumbua wachezaji wa Chelsea kwasasa ni kuelewa mfumo wa kocha Maurizio Sarri ambaye hana muda mrefu haswa katika kuzuia mashambulizi na kukaba.

Kocha Sarri anatumia zaidi mfumo wa 4-5-1 au 4-4-2 wakati klabu ikiwa inazuia huku ikitengeneza nafasi ya mita 15 kati ya walinzi na viungo na kutumia mfumo wa kukaba kuanzia juu jambo ambalo bado kwa wachezaji wa Chelsea inawachukua muda kulielewa.

Lakini pia ugumu unaongezeka kwa upande wa Chelsea kutokana na rekodi iliyokuwa nayo ikicheza dhidi ya Newcastle kwenye uwanja wa St. James' Park, rekodi zinasema katika michezo mitano ya mwisho ambayo Chelsea imecheza kwenye uwanja huo, imefanikiwa kuondoka na sare moja huku ikipoteza michezo minne.

Muda:
Saa 6:00 Jioni (Saa 18:00) Kwa saa za Afrika Mashariki

No comments:

Post a Comment