Chelsea inafanikiwa kupata ushindi katika mchezo wake wa tatu wa ligi kuu Uingereza uku ikivunja rekodi mbovu iliyokuwepo kabla katika uwanja wa St. James' Park. Katika uwanja huo, Chelsea haikuwai kupata ushindi toka mwaka 2011 ikipoteza michezo minne na kutoka sare katika mchezo mmoja tu.
Magoli ya Eden Hazard na jengine alilojifunga nyota wa Newcastle yanaifanya Chelsea kuondoka na ushindi wa magoli 1-2 huku kocha Sarri akifanikiwa kupata ushindi katika mchezo wa tatu mfululizo katika ligi kuu Uingereza.
Mchezo huo uliisha kwa dakika 45' za kipindi cha kwanza kwa sare ya 0-0 kabla ya kufanikiwa kupata goli lake la kwanza kupitia kwa nyota wake, Eden Hazard aliyefunga kwa mkwaju wa penati kabla ya dakika kadhaa baadae Newcastle kusawazisha kupitia kwa nyota wake Joselu lakini Mungu akasaidia Chelsea ikaongeza goli la pili kupitia kwa goli la kujifunga Yedlin.
Uchambuzi;
Chelsea inaonekana kuanza kuuelewa mchezo na mfumo wa kocha Maurizio Sarri ingawa tatizo bado linaonekana kwenye swala la ufungaji na ushambuliaji. Katika kipindi cha kwanza, Chelsea ilipiga shuti moja tu lililolenga golini licha ya kumiliki mpira kwa kiasi kikubwa.

Rekodi zilizowekwa;
1. Kocha Maurizio Sarri anafanikiwa kushinda michezo mitatu ya mwanzo ya ligi kuu akiungana na makocha wengine wanne waliowai kuifundisha Chelsea waliowai kupata ushindi katika michezo hiyo mitatu (Jose Mourinho, Carlo Ancelotti, Robert Di Matteo na Antonio Conte)

2. Eden Hazard anafanikiwa kufunga magoli 70 na kuingia kwenye orodha ya wachezaji watatu waliofunga magoli mengi katika ligi kuu Uingereza kwa klabu ya Chelsea. Waliofunga magoli mengi dhidi yake ni Didier Drogba aliyefunga magoli 104 na Frank Lampard aliyefunga magoli 143.
3. Jorginho Frello amefanikiwa kupiga pasi zilizofika 158 kati ya pasi 173 na kufanikiwa kupiga pasi nyingi zaidi kuliko Newcastle United ambao wao wamepiga pasi 131 katika mchezo huo wa leo.
4. Goli la Eden Hazard linatimiza goli la 250 kuwai kufungwa na Chelsea dhidi ya Newcastle united katika michuano yote.
5. Mlinzi wa Chelsea, Cesar Azpilicueta amefanikiwa kukamilisha mchezo wa 200 katika ligi kuu Uingereza toka amejiunga na Chelsea mwaka 2012.
No comments:
Post a Comment