Chelsea yawasurubu Nyuki wa London - Darajani 1905

Chelsea yawasurubu Nyuki wa London

Share This

Klabu ya soka ya wanawake ya Chelsea maarufu kama Chelsea FC Women hapo jana ilikuwa uwanjani kucheza mchezo wake wa pili wa Kombe la Continental Tyres ambapo walicheza dhidi ya London Bees au unaweza kuwaita nyuki wa London na mchezo uliisha kwa Chelsea kuondoka na ushindi wa magoli 1-6.

Magoli ya Chelsea FC Women yalifungwa na Ramona Bachmann aliyefunga mara mbili, Spence aliyefunga mara mbili pia, Fran Kirby aliyeingia kama mchezaji wa akiba na kufunga goli moja na kutengeneza jengine huku goli la sita likifungwa na Bethany England.

Huu ni mchezo wa pili wa Chelsea kupata ushindi mara baada ya wiki iliyopita kupata ushindi mwengine wa magoli 4-1 dhidi ya Brighton & Hove Albion

Mchezo unaofata ni Chelsea dhidi ya Manchester city utakaochezwa kwenye uwanja wa Kingsmeadow ambao ni uwanja wa Chelsea FC Women.

No comments:

Post a Comment