Je ni kweli Abramovich anataka kuiuza Chelsea? Ukweli wote upo hapa - Darajani 1905

Je ni kweli Abramovich anataka kuiuza Chelsea? Ukweli wote upo hapa

Share This
Kuna zengwe linaendelea kwasasa klabuni Chelsea lakini hili likihusu sana mambo ya umiliki, yaani umiliki wa klabu na hisa zake.

Toka jana kumekuwa na taarifa zikimuhusisha mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich kutaka kuiuza klabu hiyo huku ikielezwa kwamba moja ya mabenki imekabidhiwa kazi ya kumtafuta mtu atakayekuwa tayari kuinunua klabu hiyo kwa dau la paundi milioni 2 au zaidi.

Lakini baadae ikaelezwa kwamba klabu ya Chelsea imekanusha taarifa hizo kwamba hazina ukweli wowote na hakuna linaloendelea juu ya klabu hiyo kuuzwa.
Lakini Darajani 1905 tuna mashaka katika hili, tukiangalia mambo yanavyoenda klabuni inaonyesha ni dhahiri ni muda wa wakati tu kumfanya tajiri huyo akaiweka sokoni klabu hiyo.

Mambo gani?
1. Kama unakumbuka vyema katika fainali ya Kombe la FA msimu uliomalizika wa 2017-2018, tajiri huyo hakuonekana uwanjani wakati Chelsea ilipocheza dhidi ya Manchester united lakini ikaja kubainika kwamba sababu ya kutokuonekana kwake ni kutokana na kibali.chake kuishi nchini Uingereza. Lakini mpaka hii leo inaelezwa kwamba mmiliki huyo hajarejea nchini Uingereza lakini pia ameamua kusitisha mipango ya kuchukua tena kibari cha kuishi Uingereza ambapo hii inamaanisha mmiliki anakuwa mbali na klabu ilipo kwa mara ya kwanza toka mwaka 2003 alipoinunua kutoka kwa Ken Bates

2. Kama unakumbuka pia kwamba klabu ya Chelsea ilipanga kufanya upanuzi wa uwanja wake wa Stamford Bridge unaopatikana jijini London, upanuzi ambao ungeufanya uwanja kuweza kubeba mashabiki 60,000 tofauti na ilivyosasa ambapo unachukua mashabiki 40,000. Lakini baadae mara baada ya tajiri huyo kumaliza muda wake wa kuishi nchini Uingereza, mipango na mambo ya upanuzi yakasimamishwa huku klabu ikisema haitokuwa na muda maalumu wa kurejea na mipango yake ili kufanya upanuzi huo.

3. Mtifuano wa mambo ya kidiplomasia yanayotajwa kuendelea chini kwa chini kati ya Uingereza na nchi ya Urusi inatajwa pia kuwa sababu ya mmiliki huyo kuweza kuiuza klabu hiyo.

James Montague ambaye ni mwandishi wa nchini Uingereza amefanyiwa mahojiano na moja ya tovuti za michezo na kusema anaamini sio swala la kama mmiliki huyo ataiuza klabu hiyo ila ni swala la muda gani ataiuza akisema anaamini Abramovich hatokuwa tayari kuendelea kuimiliki klabu hiyo.
Nini kitaendelea katika hili? Kila litakalojiri basi Darajani 1905 tutakuwa tayari kukujuza.

No comments:

Post a Comment