Gary Cahill atoa neno kuhusu usajili wake wa kuondoka Chelsea - Darajani 1905

Gary Cahill atoa neno kuhusu usajili wake wa kuondoka Chelsea

Share This

Mlinzi wa Chelsea, Gary Cahill amekuwa akihusishwa kutakiwa na klabu kadhaa uku klabu ya Galatasaray kutoka nchini Uturuki ikitajwa kumuwania nyota huyo aliyekabidhiwa mikoba ya unahodha toka alipoondoka gwiji wa Chelsea, John Terry.

Lakini nyota huyo amekuwa hana uhakika wa kupata nafasi katika kikosi cha sasa hivi kilichochini ya kocha raia wa Italia, Maurizio Sarri ambaye amekuwa akiwatumia zaidi Antonio Rudiger na David Luiz katika safu ya ulinzi.

Jambo hilo la kukosa nafasi lilitajwa kama moja ya vichocheo vilivyomfanya muingereza huyo kulazimisha usajili wa kuondoka klabuni Chelsea.

Lakini sasa kuna taarifa mpya ambayo.imedai kwamba nyota huyo hana mpango wa kuondoka Chelsea na badala yake anajipanga kupambania namba na kusalia klabuni Chelsea.

Nyota huyo amekuwa katika miaka ya dhahabu klabuni Chelsea kutokana na kujumuishwa kwenye michezo ambayo Chelsea imeshinda mataji. Ligi kuu Uingereza, Klabu bingwa barani Ulaya, Europa League, Kombe la FA lakini pia na hata Kombe la ligi.

No comments:

Post a Comment