Nyota wa kikosi cha Chelsea raia wa Uholanzi, Marco van Ginkel ameanza mazoezi ya kujiweka sawa ili kurejea uwanjani.
Nyota huyo anayecheza nafasi ya kiungo alipata majeraha yaliyosababisha kufanyiwa upasuaji wa mguu na sasa anaweza kurejea uwanjani muda wowote kuanzia sasa.
Kupitia mtandao wa Instagram, nyota huyo alituma ujumbe wa picha ya video ikimuonyesha akiwa kwenye gari akielekea mazoezini.
Nyota huyo alitumika kwa mkopo msimu uliopita kwenye klabu ya PSV ya nchini kwao Uholanzi ambapo alifanikiwa kutwaa taji la ligi kuu akiwa na klabu yake hiyo.
No comments:
Post a Comment