Mwamuzi Lee Mason mwenye umri wa miaka 46 mzaliwa wa Bolton nchini Uingereza amechaguliwa kuwa mwamuzi katika mchezo unaokuja wakati Chelsea itakapokuwa nyumbani kucheza dhidi ya Afc Bournemouth.
Mason alikuwa mwamuzi katika michezo miwili msimu uliopita wakati Chelsea ilipokuwa uwanjani ambapo alikuwa mwamuzi katika mchezo dhidi ya Bournemouth, lakini pia akawa mwamuz katika mchezo ulioacha doa kwa klabu ya Chelsea, mchezo dhidi ya Huddersfield Town.
Mwamuzi huyo ndiye aliyesababisha Chelsea ikaadhibiwa msimu uliopita kutokana na wachezaji kumzonga kumlalamikia kutokana na kumaliza mpira wakati ambao Willian Borges alikuwa akijiandaa kupiga kona akapuliza filimbi kuashiria muda wa mapumziko wakati nyota huyo alikuwa bado hajapiga kona.
No comments:
Post a Comment