Mapema mwaka huu kulitolewa habari na klabu ya Chelsea ikiseama kwamba imeamua kusitisha mipango yake ya upanuzi wa uwanja wa klabu hiyo, Stamford Bridge uku ikisema haitoweka wazi mipango ya ujenzi huo itafunguliwa tena siku gani.
Lakini hii leo kumetolewa taarifa na moja ya vyombo vya habari nchini Uingereza kwamba klabu hiyo itaendelea na mpango wa upanuzi huo kabla ya mwaka huu kuisha uku mmiliki wa klabu hiyo, Roman Abramovich ikiaminika hana mpango wa kuiuza klabu hiyo
Uwanja huo unaopatikana jijini London nchini Uingereza ambao kwasasa unachukua mashabiki 40,000 unatarijiwa kujengwa ili kuchukua mashabiki 60,000 unatarajiwa kuigharimu Chelsea kiasi cha paundi bilioni 1.
Mwishoni wa wiki iliyopita kulitoka taarifa ya ghafla kwamba klabu ya Chelsea imewekwa sokoni na tajiri huyo wa kirusi kabla ya baadae kutolewa taarifa na klabu ya Chelsea kwamba hakuna ukweli juu ya taarifa hizo.
No comments:
Post a Comment