Nyota wa kikosi cha Chelsea raia wa Uingereza, Gary Cahill ametangaza kustaafu soka kwa upande wa timu yake ya taifa aliyoitumikia katika michezo 61 huku akiifungia magoli 5.
Mlinzi huyo mwenye miaka 32 amechukua maamuzi hayo mara baada ya kuiongoza timu hiyo katika michuano ya Kombe la Dunia iliyofanyika huko nchini Urusi yaliyoanza mwezi Juni na kumalizika mwezi Julai uku timu yake ya Uingereza ikifanikiwa kucheza hatua ya nusu fainali na kupoteza kwenye mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu ambapo walipoteza mbele ya timu ya Ubelgiji.
Cahill amekuwa akiiongoza timu hiyo mara kadhaa akiwa kama nahodha wa kikosi hicho hicho maarufu kama Simba Watatu (Three Lions).
No comments:
Post a Comment