Haya ndiyo aliyoyazungumza Ranieri mara baada ya kurejea Chelsea - Darajani 1905

Haya ndiyo aliyoyazungumza Ranieri mara baada ya kurejea Chelsea

Share This

Jana ilikuwa ni siku ya ugeni pale klabuni Chelsea ambapo klabu hiyo ilimpokea aliyewai kuwa kocha wa klabu hiyo mnamo miaka ya 2001 mpaka alipoondoka mwaka 2004, Claudio Ranieri ambaye aliachia majukumu ya ukocha klabuni hapo muda mfupi tangu tajiri raia wa Urusi, Roman Abramovich alipoinunua klabu hiyo kutoka kwa tajiri wa kiingereza, Ken Bates.

Kocha huyo ambaye aliisaidia klabu ya Leicester city kutwaa ubingwa wao pekee wa ligi kuu Uingereza msimu wa 2015-2016 alifika kwenye kiwanja cha mazoezi cha Chelsea kinachojulikana kama Cobham Training Centre na kukutana na kocha Maurizio Sarri pamoja na benchi lake la ufundi pamoja na  wachezaji akiwemo Danny Drinkwater ambaye aliwai kumfundisha pindi alipokuwa klabuni Leicester city kabla ya Chelsea kumsajili.

Kocha huyo ambaye naye pia na raia wa Italia kama ilivyo kwa Maurizio Sarri alipata wasaa wa kufanyiwa mahojiano na kusema anafikiri kufika kwa kocha Maurizio Sarri klabuni Chelsea kunaweza kuisaidia Chelsea kwa kiasi kikubwa kutengeneza soka lenye asili yake.

Lakini pia hakucha kumzungumzia kocha msaidizi, Gianfranco Zola ambaye alikuwa mchezaji wa zamani wa Chelsea na kusema anaamini ukomavu wa kocha huyo msaidizi utakuwa na msaada mkubwa na utawasaidia kwa ukubwa wachezaji wa Chelsea kwa kufundishwa na kocha anayejua nini maana ya mpira.

Jambo ambalo huenda hulijui ni kwamba Ranieri alimfundisha Zola katika klabu ya Napoli na Chelsea kwa misimu tofauti.

No comments:

Post a Comment