Nyota na kinda wa klabu ya Chelsea, Ike Ugbo amekamilisha uhamisho wake wa kujiunga kwa mkopo na klabu ya Scunthorpe United ya nchini Uingereza inayoshiriki League One.
Ugbo mwenye miaka 19 alijiunga na akademi ya Chelsea na kujumuishwa kwenye kikosi cha vijana wenye umri chini ya miaka 10 alicheza kwa mkopo msimu uliopita akiwa na klabu za Barnsley na MK Dons.
Alijiunga na Barnsley mwanzoni mwa msimu uliopita na kufanikiwa kucheza michezo 15 na kuifungia goli moja kabla ya kupelekwa tena kwa mkopo kwenye klabu ya MK Dons ambapo huko napo alicheza michezo 15 na kuifungia magoli mawili lakini akionekana kuwa mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa mara baada ya kuisaidia kikosi cha vijana kushinda taji la Ulaya (UEFA Youth League).
Ugbo anacheza nafasi ya ushambuliaji na amekuwa akitajwa kama moja kati ya washambuliaji wanaoweza kufanya makubwa sana hapo baadae.
No comments:
Post a Comment