Chelsea inashiriki michuano minne msimu huu ambayo ni ligi kuu Uingereza, Ligi ya Ulaya (Europa League), Kombe la FA na Kombe la Ligi ambalo kwa msimu huu linatambulika kama Carabao Cup.
Katika Carabao Cup jana kulifanyika upangwaji wa michezo ya raundi ya tatu huku Chelsea ikipangwa kuchezwa dhidi ya Liverpool ambayo itakuwa nyumbani kucheza mchezo huo.
Mchezo huo haujapangwa tarehe na muda maalumu wa kuchezwa lakini itakuwa kati ya tarehe 25 au 26 mwezi Septemba mwaka huu uku ukipangwa kuchezwa kwenye uwanja wa Anfield.
Wakati Chelsea ikipangiwa kuchezwa dhidi ya Liverpool, uko Manchester united inayofundishwa na kocha wa zamani wa Chelsea imepangwa kuchezwa dhidi ya Derby County inayofundishwa na aliyekuwa mchezaji wa zamani wa Chelsea, Frank Lampard.
Kwa hivyo mchezo huu utawakutanisha magwiji wa zamani wa klabu moja lakini mmoja alikuwa kocha wakati mwengine alikuwa mchezaji. Nini kitajiri?
No comments:
Post a Comment