Rasmi; Brown atolewa kwa mkopo - Darajani 1905

Rasmi; Brown atolewa kwa mkopo

Share This

Nyota na kinda wa Chelsea, Isaiah Jay Brown au kwa ufupi anaitwaga Izzy Brown amekamilisha uhamisho wake wa mkopo wa kujiunga na klabu ya Leeds United inayoshiriki lig daraja la kwanza nchini Uingereza maarufu kama Championships.

Chelsea imemtoa kwa mara nyengine tena kwa mkopo nyota huyo ambaye msimu uliopita alikuwa akiichezea klabu ya Brighton & Hove Albion lakini pia alishatolewa kwa mkopo kwenye klabu kama za Vitesse, Rotherharm na Huddersfield Town.

Nyota huyo mwenye miaka 21 alijiunga na Chelsea mwaka 2013 akitokea klabu ya West Bromwich Albion na ni raia wa Uingereza.

No comments:

Post a Comment