Nyota na winga wa Chelsea, Eden Hazard hajafanikiwa kuanza katika mchezo wowote katika michezo yote toka nyota huyo arejee klabuni Chelsea. Toka amerejea tarehe 6-Agosti, Chelsea imecheza michezo mitatu, lakini katika michezo yote amekuwa akiingia kama mchezaji wa akiba lakini inaaminika nyota huyo hatotumika tena kama winga katika kikosi cha Chelsea kwa msimu huu wakati klabu hiyo ikiwa chini ya kocha Maurizio Sarri.
Hayo ni maoni ya mchambuzi wa soka Danny Higginbotham ambaye anadai nyota huyo atabadilishwa nafasi kutoka kuwa winga mpaka mshambuliaji wa kati asiyecheza sana kama mshambuliaji asilia (false no. 9).
Mchambuzi huyo anasema anaamini kocha Maurizio Sarri atafikia maamuzi ya kumbadilisha nafasi winga huyo kama alivyofanya kwa Dries Mertens klabuni Napoli pindi kocha Sarri alipokuwa kocha wa klabu hiyo.
"Kocha Sarri anapenda mpira wenye pasi fupi na unaonda kwa kushambulia kwa haraka sana, hivyo kwangu mimi naamini atamtumia Hazard kama mshambuliaji wa kati (false no. 9) kama alivyofanya kwa Mertens kule Napoli"
"Namuona Hazard akicheza vyema sana katika mfumo huo" amesema mchambuzi huyo.
Hazard aliwai kutumika kwenye nafasi hiyo pindi klabu ilipokuwa inaongozwa na kocha Antonio Conte, lakini mara baada ya kurejea kwa Alvaro Morata na Olivier Giroud basi winga huyo alirejeshwa kwenye nafasi yake.
"Hata Pedro na Willian wanaweza kutumika kwenye nafasi hiyo" alimalizia mchambuzi huyo.
Chelsea itakuwa uwanjani jumapili hii ikicheza dhidi ya Newcastle united kwenye uwanja wa St. James' Park.
No comments:
Post a Comment